Thursday, August 23, 2012

Prezzo Amfuata Goldie Abuja

Sio rumours tena ila kwa sasa ni official. yakwamba Prezzo ametia maguu Nigeria kwa dhumuni la kurudi na Goldie ambae walikutana Bondeni pale kwa mzee Madiba katika jumba lenye kila aina ya vituko hapa nazungumzia Big Brother Africa Stargame(BBA) ya mwaka 2012.Kumbuka kua uhusiano wao ulianzia kwenye jumba hilo na kama ulikua unafuatilia shindano hilo la BBA utagundua kua wawili hao japo kua walikua wanauhusiano ila uhusiano wao uligubikwa na mizengwe na migongano mingi mno,Lakini hapa mshindi huyu wa nafac ya pili wa Shindano hilo toka 254 ameonesha kua yupo makwelini zaid



prezzo press conference

Prezzo alitumia nafac hiyo kuwaomba Radhi waNigeria kwa matukio ambayo alikua akimfanyia Goldie ndani ya Jumba hilo Tukio hilo pia lilikua likitangazwa kupitia TV ya Taifa ya Nigeria,Mkali huyo toka Kenya amesisitiza kua hakuenda Nigeria kucheza bali ameenda kwa malengo maalum,lakini pia alisema kua ili ushindi wake utimie basi apate msamaha toka kwa Goldie na ikiwezekana afunge nae pingu hadi naandika habar hii Goldie hajatoa tamko lolote juu ya hili.
Katika hatua nyengine Prezzo ambae aliondoka toka Nairobi Kenya siku ya Ijumaa kuelekea Abuja alionekana kweli anania ya kumtwaa mrembo huyo nakupata Baraka na msamaha wa wanigeria alidondoka Dresscode ya Nigeria.
Je Goldie atamsamehe Prezzo?Je?akimsamehe ndoa itafungwa?

.

0 comments:

Post a Comment