Aug 3 2012 Dogo Janja alikiri kwamba mpaka wakati huo bado alikua hajaonana na Madee toka alipoondoka Tiptop lakini angependa kuonana nae na kuzungumza nae kama kaka, vilevile aliitumia hiyo nafasi kufuta maneno ya hasira aliyoyasema June 15 2012 wakati alipokosana na Madee na kuamua kurudi nyumbani kwao Arusha ambapo alisema hata siku moja hatomtafuta Madee wala kumpigia simu kutokana na kumuharibia maisha yake kimuziki.
Baada ya kuitoa hiyo kauli Aug 3 kuhusu kutaka kuonana na Madee, juzi Aug 15 Janja amemaliza mjadala kwa kusema kama ikitokea akahitajika kufanya tena kazi za kisanii kwa kushirikiana na Madee (kolabo) yuko tayari wakati wowote.
Alisema “mi niko poa kabisa sina tatizo na mtu kwa sababu mimi naangalia mbeleni kuna nini na pia naumiza kichwa sana ili watanzania niwape vitu vipya, wapate burudani ya ukweli kutoka kwa Dogo Janja, umoja ni nguvu”
0 comments:
Post a Comment