Habari za kuamika kutoka kwa vyanzo mbalimbali zinadai
kuwa wasanii wa mkoa wa Tanga wamelikataa wazo la mbunge wa Kigoma Kaskazini
Zitto Kabwe la kufanya wimbo wa pamoja kama Tanga All Stars kwa madai kuwa
mradi huo anaufanya ili kujinufaisha kisiasa.
Hivi karibuni Mheshimiwa Zitto alikiri kuutaka urais wa
Tanzania wakati wa mahojiano na kipindi cha Makutano na watu wengi
wamekichukulia kitendo cha kuwa karibu na wasanii wa Tanzania kama njia ya ya
kujiimarisha kisiasa na kuwashawishi vijana walio wengi nchini.
Uptowntz imeongea na MwanaFA kwa simu leo (August 17)
ambaye amesema wasanii wa Tanga wana program yao wenyewe iliyopo tangu muda
mrefu na wamewahi hata kufanya show za ndani na nje.
Amesema hawawezi kujiingiza kwenye mradi huo wa Zitto
kwakuwa umekaa kisiasa zaidi.

Kigoma All Stars
mwezi
uliopita, Zitto alidai kuwa lengo lake ni kila mkoa kuwa na wimbo wa nyota wenye
asili ya mikoa mbalimbali na baada ya Kigoma mkoa wa pili aliokuwa anafanya nao mazungumzo ni Tanga ambao tayari wamemtosa.
Wakati Tanga ikishtukia mchezo huo wenye harufu ya
siasa, wasanii wa Morogoro chini ya Afande Sele tayari wameingia mkenge na
wamefanya wimbo wa Morogoro All Stars.
Morogoro All Stars inaundwa na Afande Sele, Koba,
Stamina, Belle9, Samir, Criss Wamaria, Nassa, Oten, Dayna na Zilla!
Chanzo kimoja cha uhakika kimeiambia Uptowntz kuwa
mradi wa Kigoma All Stars umegharimu mamilioni ya shilingi.

Amedai kuwa kwenye show ya wasanii hao iliyofanyika mwezi
uliopita mkoani Kigoma kila msanii alilipwa si chini ya shilingi milioni moja.
Aidha
Mheshimiwa Zitto aliwahi kudai kuwa Kigoma All Stars itakuwa kampuni na
inajenga kituo cha kuendelea vijana wenye vipaji mbalimbali mkoani
Kigoma.
Kufuatia wasanii wa Morogoro kuja na wimbo wao kama wale
wa Kigoma, kumekuwepo na hisia tofauti juu ya miradi hiyo ya wasanii kujiunga
na kutoa nyimbo za mikoa ambapo wapo wanaosema ni kitu kizuri huku wengi wakidai
inaonesha jinsi watu walivyoishiwa na mawazo mapya.
“Uvivu wa fikra na maisha ya kuiga...wangeweza kufanya
kitu nyingine nzuri ya kibunifu kuliko ku-kopi na kupest kila
kukicha tunalala na kuamka kushughulika idea ambayo tayari wenzetu washachomoka
nayo..lets not waste time on the same thing always while we can think in wide
angle and come up with moe amazing things in the Industry...ghosh....!!!,”
alisema mchangiaji aitwaye Likati.

Mwana FA
0 comments:
Post a Comment