Baada ya kumiliki gari ya kawaida aina ya Toyota
Corolla, producer na msanii wa Nigeria J Martins, ameamua kufumba macho na kununua
mikoko miwili ya gharama za kuangusha shavu chini Rolls Royce Phantom na Mercedes
Benz G-Wagon.
![]() |
Rolls Royce Phantom (Makadirio ya bei yake dola 470,295) |
G-Wagon ipo kwenye meli tayari ikipelekwa nchini Nigeria
na masuala ya makaratasi yanachelewesha usafirishwaji wa Rolls Royce Phantom
ambayo tayari ameshailipia.
![]() |
Mercedes Benz G-Wagon (Makadirio ya bei yake dola 128,535) |
Kwa sasa yupo nchini Marekani ambako anachukua kozi maalum
ya masuala ya utayarishaji wa muziki jijini New York.
Akiongea na mtandao wa Showtime, aliweka wazi kuwa
aliondoka Nigeria July 3 kwaajili ya kozi hiyo ya miezi mitatu.
0 comments:
Post a Comment