Fareed Kubanda aka Fid Q kesho ataachia video ya wimbo wake
mpya uitwao ‘Sihitaji Marafiki’ aliomshirikisha mwanadada Yvonne.
Video hiyo imefanywa na kampuni ya Showbiz Defined
iliyochini ya Mike T.
Huenda video hiyo inaweza kurudisha heshima ya kampuni ya
Showbiz ambayo hivi karibuni ilikuwa kwenye vita kali kutokana na Mike T
kutupiana maneno na director wake wa zamani, Eryne Epidu.
Ugomvi huo ulipelekea Epidu arudi kwao Uganda na kudai kuwa
Mike T alimchomea kwa uhamiaji.
Naye Ngosha The Don mwishoni mwa mwezi uliopita alitangaza
kuwa ile show yake ya online ya Fid Style Friday itaanza kuoneshwa rasmi kwenye
TV za Afrika Mashariki mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment