Wednesday, August 22, 2012

Mariah Carey Hamtaki Nicki Minaj kua Jaj.

 Siku za hivi karibuni Mariah Carey alichaguliwa kua Jaji wa msimu wa 12 wa Shindano la American Idol ambalo linatarajiwa kuanza Rasmi Januari 2013.Kuteuliwa kwa mkali huyo mke wa Nick Cannon kumetokana na kujiengua kwa Jaji ambao amedumu kwa muda mrefu katika safu hiyo ya majaji.Hapa namzungumzia Jenifer Lopez.
Siku chache kabla ya leo muaandaaji wa Shindano hilo alimpigia simu Jaji huyo mpya wa American Idol Mariah kumjulisha kua wapo katika hatua za mwisho za kumalizana na First Lady wa YMCMB Nicki Minaj ili aweze kuungana nae katika safu ya majaji.katika kile ambacho hakikutarajiwa Mariah alikata simu na kitendo hiko kimetafsiriwa kua Mariah amechukia na uteuzi /pendekezo hilo la kuwepo Rapa huyo wa kike katika safu ya majaji.
Mwaka 2010 Mariah alishawahi kufanya ngoma akimshirikisha Nicki Minaj.sasa Swali ni kwamba kwann anachukia uteuzi wake?

0 comments:

Post a Comment