Msanii wa kizazi kipya Ommy Dimpoz amefunguka sababu zilizomfanya atoke
kwenye kundi la muziki wa kizazi kipya lilokuwa likiongozwa na Tid
.Alisema Hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na mwandishi wa www.uptowntz.blogspot.com kuhusu kile kinachodaiwa kutoka kwenye kundi hilo bila ya
kuwa na maelewano na muanzilishi wa kundi hiyo
Alisema kuwa
ameamua kutoka kwa sababu aliona ni wakati wake kutangaza jina lake
pamoja na kukua kimuziki “Nimekaa kwa Tid kwa miaka mitano bila ya
mafanikio yoyote na hakuna mtu aliyekuwa anamjua Dimpozi na wala
kumsikia “ alisema
Dimpozi anazidi kufunguka kuwa baada ya
kutoka kwenye kundi hilo alipata mafanikio kwa haraka na ameweza
kujitangaza kimuziki na kupata maendeleo kutokana na muziki anaoufanya
.Anasema kuwa hana bifu na msanii yoyote na anamshukuru Tid kwa pale
alipomfikisha
0 comments:
Post a Comment