Saturday, October 25, 2014

OMY NI ZAIDI YA JINA KUBWA HAPO MBELE


ANAITWA OMY
Ukizungumzia wasanii wakubwa hapa Tanzania basi utawataja wengi ambao hujui mwanzoni walianzaje changamoto walizozipitia etc, wengine walisafiri umbali umrefu kufuata Studio zilipo kwa nauli za kuunga unga,Wengine walilala njaa na wengine walitembea umbali mrefu kwa miguu ili kukamilisha ahadi ya kurekodi aliyoahidiwa na mtayarishaji.Pamoja na yote hayo jambo moja muhimu wadau tunatakiwa kuzingatia ambalo ni kuwapa Sapot vijana wenye vipaji ili kuweza kuonesha na kuendeleza vipaji vyao mwisho wa siku iwe ajira kwao.

KAZI YAKE?
 Ni kijana ambae anafanya kazi ya Udereva katika moja ya makampuni ya Gari za kitalii visiwani Zanzibar,
Pengine sababu ni mimi au wewe na mwengine ndio maana Omy hadi leo amebaki katika kazi yake hiyo niliyoieleza hapo juu.
Kama mimi na wewe tungeweka masikio yetu vizuri na kusikiliza kazi za Omar/Omy kupitia kipaji chake cha sauti mashairi na ghani zenye mvuto wa haja kupitia mziki aufanyao wa kizazi kipya a.k.a Bongo Flava, basi leo hii Omy angekua ni miongoni mwa wasanii wa kubwa sana hapa nchini na kuipeperusha vizuri sana bendera ya nchi hii kimataifa,pengine zaidi ya hao ambao tumewaamini na kuwapa Sapot kubwa zaidi,



MZIKI WAKE,
Ameshawahi kufanya kazi kadhaa katika Studio mbali mbali visiwani zanzibar na pia nyimbo zake kuchezwa na baadhi ya Vyombo vya habari visiwani humo, Studio kama Six Records ambazo zimepa mkataba kijana huyu ni moja kati ya Studio kubwa hapa Visiwani Zanzibar


Nikuambie kitu mdau/Mshabiki mpenzi wa Bongo music bado hujachelewa unaweza kuwekeza kwa kujina huyu kupitia mziki ana kipaji na anajua kufanya muzic wa aina aifanyayo.


Leo niishie Kesho ntakupatia nafasi usikilize kupitia hapapa moja ya kazi zake, Huyu ni zaidi ya msanii mkubwa hapo baadae.





0 comments:

Post a Comment