
Friday, August 31, 2012
MARTIN KADINDA AWASILI NDANI YA NEW YORK
The young designer kutoka hapa bongo ambaye alipata mwaliko wakwenda nchini marekani katika Edition ya Africa New York fashion weekambayo yanafanyika nchini marekani.Namzungumzia Martin kadinda ameshawasili rasmi leo nchini marekani kwa ajili ya mwaliko huu wa Africa New York fashion week ambayo yatafanyika hii leo katika mji wa New York nchini marekani
Thursday, August 30, 2012
Linex,Suma Lee na Baba Levo wapata ajali

Linex,Suma Lee na Baba Levo wapata ajali ya Gari walipokua njiani kuelekea kigoma kufanya show Kigoma

akizungumzia ajali hiyo Linex amesema hawakua ktk mwendo kasi bali ajali hiyo imesababishwa na basi la abiria lililokaa kati kati ya barabara na hivyo Suma lee ambae ndo alikua Dereva wa gari hilo ameamua kulikwepa ndipo gari likaacha njia.
Wednesday, August 29, 2012
T.I.D MBARONI TENA.MARA HII IKIDAIWA ANATAKA KUMUUA ALI KIBA soma hii hapa.
Baada ya kuhojiwa na polisi kwa saa nane,mwanamke ambae anashutumiwa kutaka kumuua Ali Kiba, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.
Upande wa pili wa Shilingi haya ndio yaliyosemwa T.I.D amesema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani? toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi,nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe”
meneja wa Ally Kiba nae amesema haya“hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari kwa sasa hivi tuwaachie polisi wafanye kazi yao kwanza”
Habari zinazidi kueleza kua mwanamke huyo pamoja na watu wengine ambao wametumwa kukamilisha zoez hilo hawatokei mkoa wa Dar es salaam bali wameingia Dar kwa kaz hiyo tu.Bado Uptowntz inaendelea na umakini wa habari hii kupata tuko hilo zima keep visit us
Sunday, August 26, 2012
AVRIL AMKOSA LINEX WA IFOLA

Siku za hivi karibuni kupitia uptowntz tuliwafahamisha kuhusu Ujio wa KEKO na nia yake ya kufanya ngoma na wakali wa Bongo kama Hamisi mwinjuma na Farid Kubabanda i mean FA&FQ.Mkali huyo toka 256 alisema kua Chaguo lake la kwanza ni FA.
Sasa leo madivas wawili wa 254 watakua Club Billcanas hapa nawazungumzia madivaz wanaotamba na ngoma ya Chokoza Avril na Marya.
Kitu kimoja uptowntz ilitaka kukifaham kutoka kwa Avril Je anataka kufanya ngoma na mkali gani hapa Tanzania Bongo land kwa Baba Ridhwani.Avril bila kuficha alimtaja kijana toka Kigoma ambae amesikika katika Chorus ya Leka Dutigite Linex kua ndio chaguo lake la kwanza.

Bahati mbaya iliyopo kua wakati leo ndio siku ya Show Linex nae atakua Kigoma katika harakati zake za kikazi kuna uwezokano mkubwa 90% ya kutokuwepo kwa kolabo hilo kati ya Avril & Linex.
Saturday, August 25, 2012
MAD ICE APIGA SHOW NGOME KONGWE OCTOBER

Kupitia ukurasa wake wa FACEBOOK Msanii ambae alitamba na ngoma kibao ambazo zilifanya vizuri hapa Tanzania ingawa kwa sasa maisha yake yapo nje ya nchi hapa namzungumzia Mad Ice amethibisha kua atapiga Show Ngome Kongwe ndani ya Visiwa vya marashi ya karafuu.
Lakini pia nilimtafuta mmoja wa wadau ambao wanaushughulikia mchongo huo kwa njia ya simu akanithibitisha juu ya hilo pia Ingawa hakutaka jina lake litajwe kupitia Uptowntz.Ni mtangazaji maarufu wa Entertainment katika moja kati ya Radio za Zanzibar.Jina tunamuhifadhi kama alivyotaka na sababu alizotoa kua bado mapema sana siku ikifika atanitafuta
Hii hapa post ya Made Ice
SPECIAL ANOUNCEMENT: Tarehe 13 October nipo ndani ya Ngome Kongwe na Afribisa band kutoa burudani kwa fans wangu wa Zanzibar. Stay tuned, more info coming soon! One Lov
Friday, August 24, 2012
Kanye kwenye Twitter: ‘I just f** her!!!

Iwe aliandika kwa utani ama vyovyote, Kanye amefanya kitu ambacho kinatarajiwa kupigiwa kelele sana. Tweet hii ameifuta sekunde chache tu baada ya kuiandika lakini watu wameinasa. Swali kwenye kila mdomo wa shabiki wake, kwanini atweet kitu kama hicho?

Hata kama anamchukulia Kim Kardashian kama ‘Perfect Bitch’ ndio aandike hivyo? Hivi karibuni Kim alisema kuwa amepungua uzito kwasababu Kanye anampiga mikasi kisawasawa, kwa tweet hiyo tumeamini! It’s crazy!!!
Thursday, August 23, 2012
Prezzo Amfuata Goldie Abuja


Prezzo alitumia nafac hiyo kuwaomba Radhi waNigeria kwa matukio ambayo alikua akimfanyia Goldie ndani ya Jumba hilo Tukio hilo pia lilikua likitangazwa kupitia TV ya Taifa ya Nigeria,Mkali huyo toka Kenya amesisitiza kua hakuenda Nigeria kucheza bali ameenda kwa malengo maalum,lakini pia alisema kua ili ushindi wake utimie basi apate msamaha toka kwa Goldie na ikiwezekana afunge nae pingu hadi naandika habar hii Goldie hajatoa tamko lolote juu ya hili.
Katika hatua nyengine Prezzo ambae aliondoka toka Nairobi Kenya siku ya Ijumaa kuelekea Abuja alionekana kweli anania ya kumtwaa mrembo huyo nakupata Baraka na msamaha wa wanigeria alidondoka Dresscode ya Nigeria.
Je Goldie atamsamehe Prezzo?Je?akimsamehe ndoa itafungwa?
.
Wednesday, August 22, 2012
AVRIL NA MARYA CLUB BILLCANAS JUMAPILI HII
Mariah Carey Hamtaki Nicki Minaj kua Jaj.
Siku za hivi karibuni Mariah Carey alichaguliwa kua Jaji wa msimu wa 12 wa Shindano la American Idol ambalo linatarajiwa kuanza Rasmi Januari 2013.Kuteuliwa kwa mkali huyo mke wa Nick Cannon kumetokana na kujiengua kwa Jaji ambao amedumu kwa muda mrefu katika safu hiyo ya majaji.Hapa namzungumzia Jenifer Lopez.
Siku chache kabla ya leo muaandaaji wa Shindano hilo alimpigia simu Jaji huyo mpya wa American Idol Mariah kumjulisha kua wapo katika hatua za mwisho za kumalizana na First Lady wa YMCMB Nicki Minaj ili aweze kuungana nae katika safu ya majaji.katika kile ambacho hakikutarajiwa Mariah alikata simu na kitendo hiko kimetafsiriwa kua Mariah amechukia na uteuzi /pendekezo hilo la kuwepo Rapa huyo wa kike katika safu ya majaji.
Mwaka 2010 Mariah alishawahi kufanya ngoma akimshirikisha Nicki Minaj.sasa Swali ni kwamba kwann anachukia uteuzi wake?
Siku chache kabla ya leo muaandaaji wa Shindano hilo alimpigia simu Jaji huyo mpya wa American Idol Mariah kumjulisha kua wapo katika hatua za mwisho za kumalizana na First Lady wa YMCMB Nicki Minaj ili aweze kuungana nae katika safu ya majaji.katika kile ambacho hakikutarajiwa Mariah alikata simu na kitendo hiko kimetafsiriwa kua Mariah amechukia na uteuzi /pendekezo hilo la kuwepo Rapa huyo wa kike katika safu ya majaji.
Mwaka 2010 Mariah alishawahi kufanya ngoma akimshirikisha Nicki Minaj.sasa Swali ni kwamba kwann anachukia uteuzi wake?
DIAMOND FT J.MARTIN

Diamond Plutnam Tayari ameshamaliza kurekodi Sehem yake katika Ngoma ambayo anatarajia kumshirikisha J.Martin wa Nigeria ambae ni Producer na Muimbaji pia.kwa Sasa mkali J.Martin yupo marekani kwa ajili ya kozi fupi ya utaarishaji wa mziki.
Katika ngoma hiyo ambayo kwa Upande wa Tanzania imefanyika MJ Rec chini ya muandaaji Makochali.
katika Hatua nyingine Diamond ameshirikiana kwa ukaribu zaid na Dancer wake ambae amesikika katika ngoma hiyo dancer huyo anajulikana kwa jina la Jose.Watanzania tunasubiri kuona kolable hilo.
KILA LA KHERI DIAMOND.
Tuesday, August 21, 2012
Miaka Saba ya Complex na Vivian.
Siku ya Tarehe 21Augost 2005.Nisiku ambayo majonzi yalitanda kwa upande wa Tasnia ya Music pamoja na Habari hapa nchini Tanzania.
Kwa upande wa Music. Producer wa ngoma kama ni Raha tu,na Nyengine kibao alifariki Duniani.hapa Namzungumzia Compex ambae pia alikua ni muimbaji wa Bongo flaver.
Upande wa Habari Waandishi na Watangazaji tuliondokewa na Vivian ambae alikua mtangazaji maarufu hapa Tanzania
Inakumbukwa vizuri na Watanzania wengi kua Ajali ya Gari ndio chanzo cha vifo vya wawili hao.wapenda nao.Mungu awape amani pale walipopumzika wapenda nao hao.ambao wamefariki Dunia pamoja.
TUNAZIDI KUNAWAOMBEA
Kwa upande wa Music. Producer wa ngoma kama ni Raha tu,na Nyengine kibao alifariki Duniani.hapa Namzungumzia Compex ambae pia alikua ni muimbaji wa Bongo flaver.
Upande wa Habari Waandishi na Watangazaji tuliondokewa na Vivian ambae alikua mtangazaji maarufu hapa Tanzania
Inakumbukwa vizuri na Watanzania wengi kua Ajali ya Gari ndio chanzo cha vifo vya wawili hao.wapenda nao.Mungu awape amani pale walipopumzika wapenda nao hao.ambao wamefariki Dunia pamoja.
TUNAZIDI KUNAWAOMBEA
Ngoma ya D'banj - Go Down Imevuja

UPTOWNTZ Imefuatilia Y Dbanj Amepata heshima kubwa ya Muda mfupi.. D Banj Alifahamika Kimataifa Kutokana na wimbo wake Wa FALL IN LAV uliokuwa Produced na Don Jazzy na pia Hivi karibuni alipata Label Kwa Kanye Magharibi a.k.a (KanyeWest) Kutokana na wimbo wake Wa OLIVER TWIST..
Walio Wengi Walidhani Kupitia Mafanikio Makubwa Dbanj Angetoa HitSong Baada Ya kuanzisha Label yake..Habari Ni Kwamba Wimbo Mpya Wa Dbanj Wa Go Down Ulivuja...Na Pia Hauna Ubora Unao Stahili
Jaribu Kuskiliza hii ndio ngoma yenyewe.D'banj - Go Down
Nicki Minaj Anamatatizo ya Kiafya

Fist Lady huyo wa YMCMB Siku za hivi karibuni amekua akipiga Show non stop katika miji mbali mbali Duniani.Show hizo zimeonekana kuanza kumuathiri kiafya.Rapa huyo ameamua kusitisha Show zake za Uingereza coz ameanza kupata matatizo ya sauti yake.
kwa mujibu wa mtandao wa HUFFINGTONE POST,Mwakilishi wake ametuma email inayosema kua Nikki atatakiwa kupumzika kuperform kwenye tamasha la siku mbili la V.FIESTIVAL.Kutokana na kile alichosema STAINED VOCAL CHORDS.Habari ambazo zimenifikia ni kwamba siku za hivi karibuni Rapa huyo wa YMCMB alifanya Show moja ya Bure jijini NEW YORK iliyodumu kwa takriban Masaa mawili.
Monday, August 20, 2012
Video:Chriss Brown amliza Rihanna.

Rihana Next Chapter Oprah
Wakati Oprah akitajwa kua ndie mtangazaji anaetisha kwa maswali ya Hisia na ya kusisimua.Time hii kamfuata mkali wa BIRTHDAY CAKE"RIHANA" Nyumbani kwake.Rihana ambae alishindwa kuvumilia na kujikuta akimwaga machozi pale alipoulizwa kuhusu maisha yake na Zilipendwa wake Chriss Brown.
Pata nafac ya kutazama mahojiano hayo hii ndio Video yenyewe.
Sunday, August 19, 2012
HAYA NDIO MATUSI YA J.MARTIN
Baada ya kumiliki gari ya kawaida aina ya Toyota
Corolla, producer na msanii wa Nigeria J Martins, ameamua kufumba macho na kununua
mikoko miwili ya gharama za kuangusha shavu chini Rolls Royce Phantom na Mercedes
Benz G-Wagon.
![]() |
Rolls Royce Phantom (Makadirio ya bei yake dola 470,295) |
G-Wagon ipo kwenye meli tayari ikipelekwa nchini Nigeria
na masuala ya makaratasi yanachelewesha usafirishwaji wa Rolls Royce Phantom
ambayo tayari ameshailipia.
![]() |
Mercedes Benz G-Wagon (Makadirio ya bei yake dola 128,535) |
Kwa sasa yupo nchini Marekani ambako anachukua kozi maalum
ya masuala ya utayarishaji wa muziki jijini New York.
Akiongea na mtandao wa Showtime, aliweka wazi kuwa
aliondoka Nigeria July 3 kwaajili ya kozi hiyo ya miezi mitatu.
Keko ndani ya Rock city.mwanza.
Rapper wa kike kutoka nchini Uganda Keko ameshawasili jijini Mwanza leo saa mbili asubuhi.
Keko ambaye hii ni mara ya kwanza kuja Tanzania, ataperform
kwenye hoteli ya Star Max.
Amesema pamoja na kuja Mwanza tayari yupo kwenye mazungumzo
na MwanaFA kwaajili ya kufanya ngoma pamoja. ‘I am big fan of Mwana FA we are actually
working out something as we speak . I am looking forward and hopefully bumping
to Fid Q when I am in Mwanza, ” amesema.
A.Y AMLETA GOLDIE WA BIG BROTHER BONGO LAND
.Goldie ambae alikua mwakilishi wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Africa 2012 amethibitisha kwamba anakuja Tanzania mwanzoni mwa September 2012 kwa ajili ya kazi moja tu.
Goldie anakuja kwa ajili ya kutimiza lengo lake la kuingia studio na kurekodi kolabo na Ambwene Yesaya a.k.a AY tu. Amesema anafurahi kujua anakuja Tanzania ambapo tayari Ay ameshamuahidi kumpeleka na kumuonyesha sehemu mbalimbali za Tanzania. Goldie ambae alifall inlove kwa Prezzo wa Kenya alimfahamu Ay kwa Prezzo ambae alikua anamuongelea sana, pia kupitia nyimbo zake zilizokua zikipigwa kwenye jumba la Big Brother na hasa wakati alipokua akigombana na Prezzo.. Big Brother alikua anapiga single ya Ay na Sauti Sol wa Kenya ya I dont wanna walk alone.