Tuesday, September 8, 2015

MAN TUZO ft SAUTI SOL.

Baada ya kufanya ngoma kali ambayo ameshirikisha mkali toka THT Barnaba boy, Man tuzo anaendelea kutoboa na kuvuka boda, kwa kufanya ngoma kali nyengine ambayo inatajwa kua ndani yake sitasikika sauti za wakali toka +254, wale wakumfanya Prezdent Obama kudance, hapa nawazungumzia Sauti Sol,


                                              Man Tuzo akiwa na Barnaba Boy
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Man tuzo ametuambia kua kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi December 2015, huku akimtaja Producer mkali na hit maker wa  Wakati ya Jaffaray ft Kasim Mganga, namzungumzia Alonem kua atahusika kusimamia mapishi ya mzigo huo.

                                                     Man Tuzo akiwa na Alonem
Mziki mtamu toka Zanzibar ni lazima kutoboa, Tukithubutu kama alivyo Thubutu man Tuzo tunaweza kutimiza malengo,
uptowntz.blogspot. kupitia Mkurugenzi wake JABIR Inapenda kumpongeza MAN TUZO kwa kuthubutu,
Tusubiri kusikiliza na kutazama mziki mtamu toka kwa Man Tuzo ft Sauti Sol.

0 comments:

Post a Comment