Kutoka visiwani Zanzibar Mkali wa miduara na tungo za ukakasi AT amesema ujuio wake mpya utakua tofauti sana ule ambao watu walizoea,
Akiongea na kituo cha Luninga cha EATV alisema kua kwa sasa inaweza kua rahisi kwa watu wanaopenda kufanya colabo nae kuwezekana sababu baadhi ya wasanii walikua wanaogopa kufanya nae Colabo kwa sababu ya Style yake ana aina yake ya mziki aufanyao.
Alithibitisha kua kazi hiyo imekamilika kwa 100% pale aliposema kua Video ya kazi hiyo imefanyika hapa hapa Tanzania na zitaonekana sehemu muhimu sana za utajiri wa rasilimiali ya nchi yetu,
Ametumia fursa hiyo pia kuwataka wasanii wengine wa tanzania kufanya Video zao hapa hapa sababu kuna maeneo mazuri sana ya kufanyia video zao na zikaonekana bora.
0 comments:
Post a Comment