Leo hii msomaji wa uptowntz.blogspot.com ningependa ufahamu udhaifu wa Msanii wa Bongo Flavar ambae anafanya vizuri kupitia kazi zake za Mziki anaoufanya. Najua wengi mtadhani kua udhaifu wake ni Wanawake!! ama mabint wazuri ndio ni kweli pia huo ni udhaifu wa Diamond ila mimi leo sitaki ni zungumzie huo. Leo nataka kuzungumzia udhaifu mwengine alionao Diamond
1.HANA BUSARA
(a)Busara humfanya mtu kuchunga mdomo wake ili asiongee jambo ambalo halina faida na halitokua busara kwa mwengine kulisikia ama kumuumiza, pia msemaji lisije kumrudia yeye mwenyewe.
Hivi juzi nilifuatilia Mahojiano ambayo alifanya na moja kati ya kituo kikubwa Cha habari hapa nchini kwetu Tanzania, kwa mtazamo wa kawaida yeye alijiona kua anajibu maswali kawaida tu lakini kwa sisi wachambuzi wa mambo maneno ambayo Diamond alikua akiyaongea ama kujibu hayakua na busara wala hamjengi na yatamrudia mwenyewe,
Upo tayari kufanya kazi na Ali Kiba.(Hili moja kati ya maswali aliyo ulizwa.)
(b)Diamond alijibu Nipo tayari kufanya kazi na msanii yeyote yule, ila tu inategemea na mziki gani ama Project gani.
Hapo jibu lilikua zuri na labusara sana,
Hapa sasa ndipo alipo alipo chafua hali ya hewa na mashabiki wake wakaanza kumdharau.
(c)Alisema yeye hana tatizo anaweza kumsadia msanii yeyote yule ambae anataka msaada wake pindi akiombwa huo msaada, ameshasaidia wasanii wengi sana wa Nigeria na hivi karibuni mtasikia macollabo mengi na wasanii wa Nigeria kama vile,Don Jaz, Dr Sid, KCEE, Mafikizolo, nakadhalika, nimesaidia watu wengi sana wa nje ya nchi itakua wapa nyumbani yupo tayari kusaidia wa hapa nyumbani.endele!!!!!!!!
2.DHARAU
(d)Diamond yeye kwa Mtazamo wake akifanya Ngoma na Alikiba eti kwamba amemsaidia Alikiba kupeleka mziki wake nje ya nchi katoa na Sababu kua eti yeye tayari mziki wake umeshavuka mipaka, Hapa mdogo wangu Diamond amekosea tena sana, Namkumbusa tu kua Mziki unapanda na kushuka leo yupo juu akifanya ngoma na wasanii wa nchi nyingine ama wa hapa ndani anasema anawasaidia. kesho na kesho kutwa yeye pia anahitaji kufanya ngoma na wasanii wengine haijalishi kua wa hapa ama wa nje ya nchi itakuaje? akishuka kimuziki itakuaje? coz mimi naamini peke yake hawezi kufanya mziki wake lazima apate ushirikiano toka kwa wasanii wengine,
3.SIFA ZA KIJINGA
(e)Kuna wasanii wa ngapi ambao walikua na majina makubwa Duniani kwa mziki wao kufika kila kona ya Dunia hii na hawakua na majigambo na sifa za kijinga kama alizonazo ndugu yetu huyu ambae hata Africa yenyewe tu kuna baadhi ya nchi hawamjui wala hawajui nyimbo zake, Lugha ya mawasiliano kimataifa ndo kwanza anajifuza,
ANGALIZO.
(f)Namuombea mungu sana mziki wake ufike mbali zaid ili awe Icon wa nchi yetu na pia atuwakilishe na kuijengea Sifa nchi yetu, Lakini kwa Mambo yalivyo akiendelea na haya bac atakua hana mda mrefu wa kuishi katika anga za mziki.
Mziki ni mashabiki na mashabiki ni mziki na hao mashabiki hubadilika kulimngana na wakati na upepo unapovuma leo huu upepo umevumia kwako kesho je?
Hii ni moja ya Comments ambazo zina mtazamo tofauti kupitia FB Toka kwa Shabiki wake.
Kaka Wille · BSS & TXN Engineer at Vodacom Tanzania
Uamzi
wako sio mbaya @Diamond tatizo lako ndugu Una sifa acha kauli kwamba
unasaidia ww sema 2 naweza fanya nae collabo co uanze sema cjui nataka
nimsaidie hyo haitaniwi sawa So change control ur words wen u talk..!!Mm
ningependa useme hv...Nipo tayari kufanya collabo na kushirikia bega
kwa bega na Ali Kiba bassi ingekuwa imetulia sana bila shaka utajifunza
kupitia comment hii...!!mm napenda sana mkielewana japo Cox wote mnajua
@Di Kiba #@i like u all..!!
0 comments:
Post a Comment