Monday, October 27, 2014

MTANZANIA WA KWANZA ATUPWA NJE YA BIG BROTHER AFRICA.

                                                              Laveda
Africa mashariki imeandamwa na hali ngumu katika shindano maarufu linaloendelea hivi sasa Big brother Africa, Tumeshuhudia washiriki wawili toka nchi jerani ya Kenya wakiaga mashindano hayo, ambao ni Sabina, pamoja na Alusa ambae jana ameyaaga mashindano hayo, Upande mwengine wa Esther toka nchi jirani ya Uganda pia ametolewa nje ya jumba hilo.

Jana usiku majira ya saa 3 hivi machungu yameingia nchini kwetu mwananadada  anaeiwakilisha Tanzania Laveda, amekosa kura za kutosha toka kwa wana Africa na wana Africa Mashariki za kuweza kumbakisha ndani ya Jumba hilo.
Jana usiku Laveda akiyaaga Mashindano.

Tumekua nyuma Watanzania kwa kutoweza kupiga kura za kutosha ili kuweza kumuokoa mrembo huyo ndani ya Jumba la kifahari.
Bado tuna kila sababu ya kuweza kuendelea kufuatilizia shindano hilo kwani tuna muwakilishi wa pili ambae bado yumo humo ndani Idris ambae kwa hali yeyote ile anahitaji Suport ya watanzania na Africa pia, ili aweze kua mshindi wa Shindano hilo na kuipeperusha Bendera ya nchi hii ya Tanzania.
Idris Muwakilishi aliebaki wa Tanzania
 Piga kura kwa wingi uwezavyo ili IDRIS wa Tanzania aweze kua mshindi.



0 comments:

Post a Comment