Msanii wa muziki wa kiza kipya Bongo Flaver anaetokea visiwani Zanzibar wenyewe pia huita Zenji Flaver Nasri wa Vanilla ambae anatamba na ngoma ya zawadi kwa sasa pia alishatoa ngoma kibao kali kama Vile Hanitaki,pia ameshafanya kazi kadhaa katika Studio za G.Records Uprise Music na Mazuu Records na kushirikiana na mastaa wa bongo kama Abdul kiba n.k.Unaambiwa msanii huyo ameonekana kuzama katika mahaba niue kwa mtoto Shinella Queen ambae pia alishawahi kutoa ngoma aliomshirikisha Jobfire wa Melody lakini pia ni Dancer na Video Queen, wawili hao walionekana maeneo ya Chukwani huko visiwani zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Starehe huko chukwani mesi Club wakiwa katika mahaba mazito.
SHINELLA QUEEN & NASRI WA VANILLA
Paparazi wetu alipo waona akatupatia picha kadhaa na akatufahamisha pia SHINELLA QUEEN ni ndugu wa msanii Jobfire ambae wanafahamiana kwa karibu na Nasri wa Vanilla, nilitaka kujua kua Jobfire amelichukuliuaje hili nimemtafuta kwa Simu hakupatikana hewani, Pia nilijaribu kumtafuta nasri wa vanilla ili aniambie juu ya matukio hayo pia hakunipa ushirikiano wa kutosha.
WAPENDANAO KTK MAHABA NIUE
0 comments:
Post a Comment