Tuesday, October 14, 2014

MZIGO MPYA WA MO MUSIC UNATOKA WIKI IJAYO.


Baada ya kufanya Vizuri sana kwa basi nenda Mo Music amefunguka kua yupo tayari kuachia ngoma nyingine mpya ambayo Inaitwa Simama, Mazuu ndio Studio ambayo imehusika katika utengenezaji wa Track hiyo. Pamoja na kua yupo tayari kuachia mkwaju huo amefunguka kua ana ngoma mbili ambazo zote kali Simama ambayo imefanywa na mazuu na Natamani ambayo imetengenezwa na Lollipop, bado hajajua ipi kati ya hizo ataiachia, hadi kufikia wiki kesho Watanzania watakua wamejua ipi kati ya hizo mbili.
Mo Mosic ameenda mbali zaidi na kuweka wazi tofauti kati ya Basi Nenda na zinazofuata, kwanza kasema Midundo, kisha Uandishi, mpangilio wa Sauti na Ufundi wa uimbaji katika ngoma zijazo.
Pia anasema hajamshirikisha msanii yeyote katika ngoma zote mbili, kwa sababu anataka kuwadhihirisha watanzania kua hakubahatisha Basi nenda bali ni kipaji endelevu na uwezo wake mkubwa wa sanaa.

0 comments:

Post a Comment