Wednesday, October 22, 2014

DIAMOND & NEY WA MITEGO MIKONONI MWA POLISI

Nyuma ya Fiesta 2014 kuna mengi sana yamejitokeza pia linatajwa kua ndio tamasha pekee lililotia fora kwa matukio tangu huu mwaka uanze, moja kati ya matukio ambayo yalileta utata na bado yanautata ni,
1.Vita ya mashabiki wa Alikiba Vs Diamond
2.Vita kati ya Clouds Fm Vs Times Fm Radio
3.Vita kati ya JWTZ Vs Diamond & Ney wa Mitego.
Tumeshasoma mengi sana yaliyoandikwa na vyombo vya habari vya hapa nchini na nje ya nchi kuhusiana na kipengele no.1.na mbili, hapo juu.
Msomaji wangu leo nataka nikupatie Inshu kubwa inayoendelea hivi sasa hapa mjini Dsm, Tunakumbuka vizuri sana wale ambao tulihudhuria Show na wale ambao tuliangalia nyumbani kupitia Luninga zetu, kua Diamond na Ney wa mitego walipanda jukwaani wakiwa na sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania,Pengine niseme Rangi ya nguo zao zimefanana na nguo za Jeshi hilo.
Habari kubwa niliyonayo leo ni kwamba Wawili hao wametakiwa kufika katika kituo cha polisi Osabay wakiwa na nguo hizo zinazofanana na sare za JWTZ,
Wakati huo huo inasemekana kua Bab Tale yeye yupo polisi tangu siku ya pili ya tukio hilo kubwa hapa nchini naizungumzi Fiests 2014.
Akizungumza kwa ufasaha kabisa Ney wa mitego amesema kua ni kweli tukio hilo ni kubwa na wametakiwa kurejesha nguo hizo kituo cha polisi Ostabay Dsm,Hakuishia hapo Ney amesema kua amepata simu kutoka kwa Diamond pia nae akitakiwa kutimiza agizo kama hilo la JWTZ,
Ney ameieleza Uptowntz.blogspot.com kua kuna watu wanayakuza haya mambo na kufanya kua na Sura mpya yeye anadhani ni ya kisheria na ya kuisha na huenda pia wakawa na makosa ya kesheria bila wenyewe kujijua. Ila yataisha tu amesema Ney. 



0 comments:

Post a Comment