TAMASHA LA ZIFF KUANZA RASMI JULAI 7-15
Mkurugenzi Mkuu wa Tamasha la Filamu za Majahazi Zanzibar (Zanzibar
International Film Festival),Prof. Ikaweba Bunting (pili kulia)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza Ufunguzi rasmi wa Tamasha hilo ambalo
linatarajiwa kuanza Julai 7 - 15 katika viwanja vya Ngome Kongwe
Kisiwani Zanzibar.Tamasha hilo kwa Mwaka huu linatarajiwa kufunguliwa na
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Mh. Dk. Ali Mohamed Shein huku Mgeni Maalum akitarajiwa kuwa
Muongozaji wa Filamu kutoka Hollywood,Mario Van Peebles aliewahi
kung'ara katika filam za American Most Wanted,New Jack City na nyingine
nyingi.Wengine pichani ni Waratibu wa Tamasha hilo,kutoka kulia ni
Muslim Nassor,Robert Monondoli na Sabrina Othman Faraji.
0 comments:
Post a Comment