Monday, July 16, 2012

HUU NDIO UJIO MPYA WA MON G

MON-G akiwa na DULLAYO. Msanii wa kizazi kipya Ally Ramandhani ‘Mon G’ wiki hii anatarajia kutambulisha wimbo mpya wa ‘Binadamu’ .Akizungumza Dar es Salaam mwisho mwa wiki hii Mon G alisema wimbo huo utaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini mara baada ya kuutambulisha wiki hii Msanii huyo alitamba kwamba wimbo huo utakuwa kivutio kwa mashabiki wa kizazi kipya kutokana na maudhui aliyoyatumia ambayo yanaelimisha jamii. Alisema wimbo huo ambao ameutunga mwenyewe una maana kubwa kwa binadamu wote si wa kuwasikiliza kwani kila mtu ana mambo yake anayoyataka bila ya kumuiga mtu . Mon G, alisema wimbo huo ambao ameurekodi katika studio ya E Motion Record, pamoja na kwamba inazungumzia mapenzi lakini pia imetungwa kwa umahiri wa kumfanya mtu apende kusikiliza mara kwa mara “Lakini pia baada ya wiki kama mbili hivi ninatarajia kuingia kwenye harakati za kuitengeneza video yake sina mpango wa kuwa na albamu kwa kuwa hazilipi “ alisema Nyimbo nyingine za msanii huyo alizozitoa awali ni Mtoto wa Dar, Damu yangu, Uko wapi na sasa amekuja na Binadamu

0 comments:

Post a Comment