Saturday, July 28, 2012
Home »
» SOPRANO ANUSURIKA KUFA
SOPRANO ANUSURIKA KUFA
Mkali wa R&B Hapa nchini Francis Ndumbaro a.k.a Soprano jana 27/7/2012 majira ya saa 4:30 Asubuhi amepata ajali maeneo ya Airport Das es Salaam.msanii huyo ambae anafanya vizuri na ngoma yake ya Happy Day alikua katika Pikipiki ya aina ya Bajaji.
Chanzo cha Ajali ni Roli la kampuni ya Azam inayomilikiwa na Bakharesa likiwa katika harakati za kuovertake Bajaji aliyopanda msanii Soprano ndipo gari hilo lilipoigonga Bajaji hiyo kwa pembeni.
Mwanamziki huyo wa kizazi kipya alikua akitokea Nyumbani kwake Kiwalani Kijiwe Samli akielekea Studio kwa Producer aliyetambulika kwa jina la AMBA iliyopo maeneo ya Njiapanda Segerea.
Mbali na msanii huyo walihusika pia watu wengine wanne katika ajali hiyo nao ni,Director wa kampuni ya kutengeneza Video ya Emedia anaitwa SAMAJAMA,wengine ni JABIR,STIVE na FESTO ambae ndio alikua Dereva wa Pikipiki hiyo aina ya Bajaji.
Wote watano walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya AMANA Iiyopo maeneo ya Ilala Dar es Salaam.
Hata hivyo msanii huyo anendelea vizuri na tayari amaesharuhusiwa kurejea Nyumbani kwake toka Hospitalini hapo.
Akichapa story na Uptowntz.blogspot.com Soprano pia alinifahamisha juu ya Ujio wake mpya baada ya Happy Day na kuwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya Track hiyo iliyosimamiwa na mkali STIVE WHITE yenye mahadhi ya zuku.Haitosh hapo nilipata nafac ya kusikiliza Demo ya Bidhaa hiyo.Honest Bidhaa ni kali.kupitia uptowntz.blogspot.com.utapata habar zaid juu ya ngoma hiyo.
0 comments:
Post a Comment