Tuesday, November 4, 2014

FID Q KUNYOA RASTA ZAKE NA HII NDIO STYLE ATAKAYONYOA. SOMA HAPA


Siku za hivi karibuni alipokua akifanya mahojiano na Clouds fm Radio kupitia kipindi cha XXL Fareed Kubanda a.k.a. FID Q alisema kua kutokana na Joto la Dar, atalazimika kunyoa Rasta zake bila kutaja Style gani ya nywele atanyoa,
Leo hii amekuja na hili jipya jengine kuhusu kunyoa nywele zake pamoja na style ya unyoaji.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Fid Q amesema yupo mbioni kupunguza rasta zake kwa lengo la kujiweka tofauti na jinsi ilivyo. Ameileza uptowntz.blogspot.com
Mwanamuziki huyo alisema kimsingi akishamaliza kupunguza rasta, atanyoa kabisa nywele zake kwa mtindo wa unga na alipoulizwa zaidi alisema anataka kujibadilisha ili aongeze pia mashabiki wake.
Alisema si jambo la kwanza kwa wasanii kuamua kubadili staili zao za mavazi au mitindo ya nywele na mara nyingi ushahidi unaonyesha kuwa kwa kufanya hivyo hata muziki nao soko lake linapanda.

0 comments:

Post a Comment