
Baada ya kufanya vizuri sana na mkwaju wa kibaba KICHEFCHEF ,msanii wa Bongo Flaver anetokea visiwani Zanzibar,ambae kwa sasa anatamba na mkwaju wa nichekeche hapa namzungumzia SMAIL,ambae pia atakuwepo katika Uzinduzi wa Album ya kiroho safi ya Sultan King siku ya Tarehe 22 Jimkana Zanzibar
Tayari kijana huyo ameshakamilisha kila ki2 kwa ajili ya kukamilisha Upigaji wa Video yake mpya ya NICHEKECHE.
Mkwaju ndo huo hapo usikilize kwanza huku tukisubiri kichupa.
Chanzo chetu cha habari kimegundua kua Tayari kampuni moja toka Dar es Salaam imeshatua hapa visiwani Zanzibar tayari kwa Shughuli hiyo.jina la kampuni tunalo tumelihifadhi.
Uchunguzi wa Chanzo chetu cha habari umegundua pia Mwanamitindo na mmbunifu wa nguo maarufu hapa Zanzibar pia ametumika katika kufanya yake katika video hiyo,Hapa namzungumzia Mr.Wise.

Mr.Wise.(wise Fasion)
Habari ambayo pia nimeipata ni kwamba Warembo watakaotumika VIDEO MODALS wametoka Dar es Salaam wakifanya kolabo na warembo wa Zenji,
Kila la kheri kijana tunatarajia kuona Video inayoendana na maandalizi Bab kubwa ambayo umeyafanya,
0 comments:
Post a Comment