
Queen kutoka tasnia ya filamu Bongo, Wema Abraham Sepetu, ametupilia mbali madai ya ‘star’ wa muziki wa kizazi kipya nchini Mohamed Hassan, ‘Moracka’ kuwa amewahi kutoka nae kimapenzi.
Akizungumza ‘live’Wema aliyewahi kushikilia ‘crown’ ya umalkia wa Tanzania amefunguka kuwa, kamwe hajawahi kufikiria kufanya jambo hilo kwa Moracka ingawa alikiri kuwa mara kadhaa nyota huyo alikuwa akimsumbua akimuomba kudondoka nae ‘on bed’..
“Ni kitambo kidogo kabla sija shinda taji la miss Tanzania, nakumbuka alikuja kuniomba kufanya nae video ya wimbo wake nafikiri hayo ndiyo yalikuwa mazungumzo yetu ya mwanzo…

kinyume na hapo tumekuwa tukizungumza kawaida na kamwe sijawahi kuthubutu kutoa nguo na kumpa mwili wangu Moracka alisema Wema.
Juzi kati kupitia kipindi kinachorushwa na TV maarufu hapa nchini Moracka alifunguka kuwa amewahi kutoka kimapenzi na wema Sepetu kitambo kabla mwanadada huyo hajanza kujiachia na watu wengine maarufu akiwemo nyota wa Bongo fleva Nassib Abdul Diamond.
0 comments:
Post a Comment