Beyonce amwandikia barua shabiki wake kipofu
Beyonce amemwandikia barua ya wazi shabiki wake Timmy
Kelly, aliyezaliwa na upofu wa macho.
Mwanamuziki huyo alikutana na Timmy kwa mara ya kwanza
wakati kijana huyo akiwa na miaka 13, backstage kwenye tuzo za Grammy.
Timmy kidogo amlize Beyonce baadaya kumwimbia wimbo wake
Irreplacable, na hamjamsahau hadi leo.
Baada
ya kubaini kuwa Timmy ambaye kwa sasa ana miaka 18 amehitimu high
school na amechaguliwa kujiunga na chuo, Bey ameandika barua ya
kumpongeza kwa hatua hiyo.
“Mara ya kwanza nimekutana na Timmy ilikuwa mwaka 2007, backstage
kwenye Grammys. Alikuwa na miaka 13 na aliugusa moyo wangu kwa sauti yake na
mapenzi yake kwa muziki na maisha,” ameandika Beyonce.
“Sasa hivi ana miaka 18 na amehitimu high school –
Najinua sasa kwake!”
"Timmy alizaliwa kipofu. Lakini hili halikumtatiza.
Amethibitisha kwa kila mmoja kuwa kila kitu kinawezekana kama ukijiamini na
kujituma.”
"Mjini Philadelphia anajulikana sana kama bahati
kwa Eagles na kila anapoimba wimbo wa taifa kwenye mchezo timu hiyo hushinda.”
0 comments:
Post a Comment