Maombi ya watanzania
pamoja na michango yao ya fedha vimesaidia kumfikisha mwigizaji Sajuki hapa
alipo baada ya kupata nafuu kubwa toka apelekwe India kuitibiwa.
Wastara akizungumza
exclusive na Jabir Super Jay kupitia ngomazetu.blogspot.com amesema Sajuki
anaweza kuanza kuigiza hata sasa kwa sababu nguvu imesharudi, anaweza kutembea
kwa muda mrefu na hata hali yake ya sasa imebadilika sana tofauti na mwanzo.
Amesema “baada ya miezi
mitatu Sajuki anaweza kuanza kuigiza kama yeye mwenyewe atapenda na hata sasa hivi
alipo pale unaweza kwenda nae location hana wasiwasi wowote ila kwa sababu ni
mtu amefanyiwa upasuaji anahitaji kupumzika zaidi huwezi kutoka nae kwa sababu
kuigiza inahitaji akili zaidi lakini baada ya miezi mitatu au minne anaweza
kuendelea na kazi zake kama kawaida”
kwenye sentensi nyingine
Wastara amesema hawezi kuzuia Sajuki kupigwa picha za Tv na magazeti kwa sababu
kupitia vyombo hivyo vya habari ndio walifahamu kwamba anaumwa na wakaamua
kumchangia sasa ni lazima wajue pia anaendeleaje kupitia vyombo hivyo hivyo.
0 comments:
Post a Comment