SHOW YA MILIONI MOJA MADEE ALINIPA CHINI YA LAKI MBILI.
Siku moja baada ya Dogo Janja kudaiwa kufukuzwa Tip Top
Connection, ukweli halisi kuhusiana na uamuzi huo umewekwa wazi na yeye
mwenyewe.
Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo
Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni.
Kwa mujibu wa interview (ya pili kufanyiwa baada ya
kipindi cha Amplifaya cha jana) tuliyofanya naye kwa simu saa moja asubuhi leo
(June 14) akiwa stand kurejea nyumbani,
uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha kuishi Dar es Salaam.
Anasema tangu aje Dar es Salaam hajawahi kusaidiwa
chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya
shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja)
alikuwa akiishi kwake.
Anasema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu
alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni
moja.
Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela
kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza
hela nyingi za show.
“Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika
kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” ameongea uchungu.
Dogo anasema ilikuwa inafikia wakati akifanya show za
ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa
halipwi kabisa.
Tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya
kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi.
“Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja,
Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” anasema.
Mpaka tunaongea naye asubuhi hii, anasema kadi yake
imebakiwa na shilingi 25,000 tu.
Ameendelea kudai kuwa juzi Madee alimpigia simu na
kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na atamlipa shilingi
laki moja.
“Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki
moja?”. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama.
Baada ya show kumalizika anasema yeye na back up artist
wake walirudishwa saa saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni
kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia.
Dogo Janja anaeleza kuwa inamuuma sana kwakuwa muziki
haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia
kimaslahi na hadi leo hii anamalizia kujenga nyumba yake.
“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune.”
Ameendelea kusema kuwa hiyo juzi sasa hadi kufikia Tip
Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita
kisha kuanza kumpiga.
Alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza
kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa
nataka kumroga. Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na amesikitika sana.”
Anasema simu yake alipewa jana.
Kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka
kurudi nyumbani ndicho kimemfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa
watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee
aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na
vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment