Nyota wa muziki wa kizazi
kipya kutoka ‘kruu’ ya Tip Top Connection yenye maskani
yake pande za Manzese jijini Dar es Salaam
Abdul Abubakar Chende ‘Dogo
Janja’ ametupiwa virago ndani ya kundi hilo.
Akizumngumza na Teentz .com
mapema leo kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally ‘Madii’ amesema
kuwa Dogo Janja ameshindwa kuendana na makubaliano
halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo
kuhudhuria shuleni kama alivyokuwa akitakiwa kufanya kila
siku badala yake amekuwa akiendekeza starehe na wakati
mwingine kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua
kundi hilo.
“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema
leo tukiwa maeneo ya Ubungo tayari kwa safari ya kurudi kwao
na wakati huo tulifanya mawasiliano na…
Nyota wa muziki wa kizazi
kipya kutoka ‘kruu’ ya Tip Top Connection yenye maskani
yake pande za Manzese jijini Dar es Salaam
Abdul Abubakar Chende ‘Dogo
Janja’ ametupiwa virago ndani ya kundi hilo.
Akizumngumza mapema leo kiongozi wa
kundi hilo Hamad Ally ‘Madii’ amesema kuwa Dogo Janja
ameshindwa kuendana na makubaliano halisi yaliyokuwepo baina yake
na uongozi wa kundi hilo ikiwemo kuhudhuria shuleni kama alivyokuwa
akitakiwa kufanya kila siku badala yake amekuwa
akiendekeza starehe na wakati mwingine kufanya mambo ambayo kwa
namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.
“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema
leo tukiwa maeneo ya Ubungo tayari kwa safari ya kurudi kwao
na wakati huo tulifanya mawasiliano na baba yake kumuarifu kuwa Tip
Top hatuko na mwanae kwa sasa” alisema Madii
Katika hatua nyingine Madii
amesema kuwa Dogo Janja alilewa sifa na kujisahau kufanya yale
anayotakiwa kufanya ndani nanje ya kundi kufuatia mafanikio ya muziki
aliyoyapata akiwa na Tip Top Connection kwani hivi karibuni alitega shule
na kwenda kujificha nyumbani kwa TundaMan hukua akimuaga Madii kuwa
anakwenda shule.
Kuona hivyo TundaMan aliamaua
kumuarifu Madii na mara moja kiongozi huyo wa kundi aliamua kwenda
kumsaka, lakini baada ya dogo Janja kugundua kuwa Madii anakuja aliamua
kukimbia na kwenda kujificha uchochoroni lakini akiwa huko mafichoni
bahati mabaya alikanyaga kuku na siri yake kujulikana
kuwa amejificha hapao ndipo alipokamatwa na kuamriwa kufungasha kilicho
chake tayari kurejea ‘kileji’.
"vimekuwa ni vitendo vya kila
mara kukacha kuhudhuria shule, tumechoka na hatukuwa na njia nyingine ya
kufanya alisema Madii'
0 comments:
Post a Comment