Thursday, June 21, 2012
BBA: Prezzo aomba arudishwe kwenye eviction
WASTARA ATOA HABARI MPYA ZA SAJUKI
Maombi ya watanzania
pamoja na michango yao ya fedha vimesaidia kumfikisha mwigizaji Sajuki hapa
alipo baada ya kupata nafuu kubwa toka apelekwe India kuitibiwa.
Wastara akizungumza
exclusive na Jabir Super Jay kupitia ngomazetu.blogspot.com amesema Sajuki
anaweza kuanza kuigiza hata sasa kwa sababu nguvu imesharudi, anaweza kutembea
kwa muda mrefu na hata hali yake ya sasa imebadilika sana tofauti na mwanzo.
Amesema “baada ya miezi
mitatu Sajuki anaweza kuanza kuigiza kama yeye mwenyewe atapenda na hata sasa hivi
alipo pale unaweza kwenda nae location hana wasiwasi wowote ila kwa sababu ni
mtu amefanyiwa upasuaji anahitaji kupumzika zaidi huwezi kutoka nae kwa sababu
kuigiza inahitaji akili zaidi lakini baada ya miezi mitatu au minne anaweza
kuendelea na kazi zake kama kawaida”
kwenye sentensi nyingine
Wastara amesema hawezi kuzuia Sajuki kupigwa picha za Tv na magazeti kwa sababu
kupitia vyombo hivyo vya habari ndio walifahamu kwamba anaumwa na wakaamua
kumchangia sasa ni lazima wajue pia anaendeleaje kupitia vyombo hivyo hivyo.
Beyonce amwandikia barua shabiki wake kipofu
Beyonce amwandikia barua shabiki wake kipofu
Beyonce amemwandikia barua ya wazi shabiki wake Timmy
Kelly, aliyezaliwa na upofu wa macho.
Mwanamuziki huyo alikutana na Timmy kwa mara ya kwanza
wakati kijana huyo akiwa na miaka 13, backstage kwenye tuzo za Grammy.
Timmy kidogo amlize Beyonce baadaya kumwimbia wimbo wake
Irreplacable, na hamjamsahau hadi leo.
Baada
ya kubaini kuwa Timmy ambaye kwa sasa ana miaka 18 amehitimu high
school na amechaguliwa kujiunga na chuo, Bey ameandika barua ya
kumpongeza kwa hatua hiyo.
“Mara ya kwanza nimekutana na Timmy ilikuwa mwaka 2007, backstage
kwenye Grammys. Alikuwa na miaka 13 na aliugusa moyo wangu kwa sauti yake na
mapenzi yake kwa muziki na maisha,” ameandika Beyonce.
“Sasa hivi ana miaka 18 na amehitimu high school –
Najinua sasa kwake!”
"Timmy alizaliwa kipofu. Lakini hili halikumtatiza.
Amethibitisha kwa kila mmoja kuwa kila kitu kinawezekana kama ukijiamini na
kujituma.”
"Mjini Philadelphia anajulikana sana kama bahati
kwa Eagles na kila anapoimba wimbo wa taifa kwenye mchezo timu hiyo hushinda.”
Thursday, June 14, 2012
WEMA SEPETU SIJALALA NA MORACKA

Queen kutoka tasnia ya filamu Bongo, Wema Abraham Sepetu, ametupilia mbali madai ya ‘star’ wa muziki wa kizazi kipya nchini Mohamed Hassan, ‘Moracka’ kuwa amewahi kutoka nae kimapenzi.
Akizungumza ‘live’Wema aliyewahi kushikilia ‘crown’ ya umalkia wa Tanzania amefunguka kuwa, kamwe hajawahi kufikiria kufanya jambo hilo kwa Moracka ingawa alikiri kuwa mara kadhaa nyota huyo alikuwa akimsumbua akimuomba kudondoka nae ‘on bed’..
“Ni kitambo kidogo kabla sija shinda taji la miss Tanzania, nakumbuka alikuja kuniomba kufanya nae video ya wimbo wake nafikiri hayo ndiyo yalikuwa mazungumzo yetu ya mwanzo…

kinyume na hapo tumekuwa tukizungumza kawaida na kamwe sijawahi kuthubutu kutoa nguo na kumpa mwili wangu Moracka alisema Wema.
Juzi kati kupitia kipindi kinachorushwa na TV maarufu hapa nchini Moracka alifunguka kuwa amewahi kutoka kimapenzi na wema Sepetu kitambo kabla mwanadada huyo hajanza kujiachia na watu wengine maarufu akiwemo nyota wa Bongo fleva Nassib Abdul Diamond.
Kanye West apost picha ya ‘utupu’ ya Kim Kardashian Twitter!!
Juzi
usiku Kanye West aliwashangaza followers wake wa
Twitter kwa kupost kwa bahati mbaya picha ya mwanamke ambaye kwa haraka
ukimwangalia utamuona anafanana na mpenzi wake Kim Kardashian.
Picha hiyo inamuonesha mwanamke akiwa amekaa kwenye kiti, akiwa uchi na akionekana akila chakula huku akiipa mgongo kamera.
Wakati sura ya mwanamke huyo haionekani full, anaonekana
kuwa kama ni mpenzi wake na Kanye, Kim.
Kwa
mujibu wa mtandao wa MediaTakeOut, Kim alichukia kwa kitendo hicho cha
Kanye kushare picha yake kwenye mtandao huo wa kijamii na
kumuomba aitoe mara moja.
Kanye aliitoa picha hiyo japo story hiyo na Kim iligeuka
kuwa mjadala mkubwa.
Kwa mujibu wa mtandao wa AceShowbiz, ilikuja kubainika
kuwa picha hiyo ni ya nyota wa picha za ngono aitwaye Amia Miley, lakini
amegoma kuthibitisha kama ni yeye.
"Apparently a naked photo of me eating is going
viral.... as Kim Kardashian.... Im confused," aliandika kwenye Twitter.
Unadhani hiyo picha ni ya Kim kweli?
UPANDE WA PILI WA SHILINGI DOGO JANJA Vs MADEE
SHOW YA MILIONI MOJA MADEE ALINIPA CHINI YA LAKI MBILI.
Siku moja baada ya Dogo Janja kudaiwa kufukuzwa Tip Top
Connection, ukweli halisi kuhusiana na uamuzi huo umewekwa wazi na yeye
mwenyewe.
Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo
Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni.
Kwa mujibu wa interview (ya pili kufanyiwa baada ya
kipindi cha Amplifaya cha jana) tuliyofanya naye kwa simu saa moja asubuhi leo
(June 14) akiwa stand kurejea nyumbani,
uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha kuishi Dar es Salaam.
Anasema tangu aje Dar es Salaam hajawahi kusaidiwa
chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya
shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja)
alikuwa akiishi kwake.
Anasema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu
alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni
moja.
Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela
kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza
hela nyingi za show.
“Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika
kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” ameongea uchungu.
Dogo anasema ilikuwa inafikia wakati akifanya show za
ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa
halipwi kabisa.
Tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya
kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi.
“Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja,
Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” anasema.
Mpaka tunaongea naye asubuhi hii, anasema kadi yake
imebakiwa na shilingi 25,000 tu.
Ameendelea kudai kuwa juzi Madee alimpigia simu na
kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na atamlipa shilingi
laki moja.
“Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki
moja?”. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama.
Baada ya show kumalizika anasema yeye na back up artist
wake walirudishwa saa saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni
kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia.
Dogo Janja anaeleza kuwa inamuuma sana kwakuwa muziki
haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia
kimaslahi na hadi leo hii anamalizia kujenga nyumba yake.
“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune.”
Ameendelea kusema kuwa hiyo juzi sasa hadi kufikia Tip
Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita
kisha kuanza kumpiga.
Alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza
kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa
nataka kumroga. Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na amesikitika sana.”
Anasema simu yake alipewa jana.
Kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka
kurudi nyumbani ndicho kimemfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa
watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee
aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na
vyombo vya habari.
DOGO JANJA ARUDISHWA KWAO
Nyota wa muziki wa kizazi
kipya kutoka ‘kruu’ ya Tip Top Connection yenye maskani
yake pande za Manzese jijini Dar es Salaam
Abdul Abubakar Chende ‘Dogo
Janja’ ametupiwa virago ndani ya kundi hilo.
Akizumngumza na Teentz .com
mapema leo kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally ‘Madii’ amesema
kuwa Dogo Janja ameshindwa kuendana na makubaliano
halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo
kuhudhuria shuleni kama alivyokuwa akitakiwa kufanya kila
siku badala yake amekuwa akiendekeza starehe na wakati
mwingine kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua
kundi hilo.
“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema
leo tukiwa maeneo ya Ubungo tayari kwa safari ya kurudi kwao
na wakati huo tulifanya mawasiliano na…
Nyota wa muziki wa kizazi
kipya kutoka ‘kruu’ ya Tip Top Connection yenye maskani
yake pande za Manzese jijini Dar es Salaam
Abdul Abubakar Chende ‘Dogo
Janja’ ametupiwa virago ndani ya kundi hilo.
Akizumngumza mapema leo kiongozi wa
kundi hilo Hamad Ally ‘Madii’ amesema kuwa Dogo Janja
ameshindwa kuendana na makubaliano halisi yaliyokuwepo baina yake
na uongozi wa kundi hilo ikiwemo kuhudhuria shuleni kama alivyokuwa
akitakiwa kufanya kila siku badala yake amekuwa
akiendekeza starehe na wakati mwingine kufanya mambo ambayo kwa
namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.
“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema
leo tukiwa maeneo ya Ubungo tayari kwa safari ya kurudi kwao
na wakati huo tulifanya mawasiliano na baba yake kumuarifu kuwa Tip
Top hatuko na mwanae kwa sasa” alisema Madii
Katika hatua nyingine Madii
amesema kuwa Dogo Janja alilewa sifa na kujisahau kufanya yale
anayotakiwa kufanya ndani nanje ya kundi kufuatia mafanikio ya muziki
aliyoyapata akiwa na Tip Top Connection kwani hivi karibuni alitega shule
na kwenda kujificha nyumbani kwa TundaMan hukua akimuaga Madii kuwa
anakwenda shule.
Kuona hivyo TundaMan aliamaua
kumuarifu Madii na mara moja kiongozi huyo wa kundi aliamua kwenda
kumsaka, lakini baada ya dogo Janja kugundua kuwa Madii anakuja aliamua
kukimbia na kwenda kujificha uchochoroni lakini akiwa huko mafichoni
bahati mabaya alikanyaga kuku na siri yake kujulikana
kuwa amejificha hapao ndipo alipokamatwa na kuamriwa kufungasha kilicho
chake tayari kurejea ‘kileji’.
"vimekuwa ni vitendo vya kila
mara kukacha kuhudhuria shule, tumechoka na hatukuwa na njia nyingine ya
kufanya alisema Madii'