Sunday, February 9, 2014
Hii ndo Video utata ya Shakira ft. Rihanna cant Remenber to forget you. itazame.
Hii ndio video ya Shakira iliyokosolewa na Mwanasiasa wa Colombia anaefahamika kwa jina la Marco
Fidel Ramirez aliedai kua inachochea usagaji na uvutaji sigara pia amesema kua inapelekea kuwaharibu watoto wa dogo kimaadili.
TAMKO LA WEUSI KUHUSU VIDEO KUCHEZWA CHANEL O

Jana ilikuwa siku nzuri kwenye historia ya muziki ya kundi la Weusi linaloundwa na wasanii watano kutoka Kaskazini mwa Tanzania, Arusha, baada ya video ya wimbo wao ‘Nje ya Box’ kuchezwa Channel O.
Joh Makini aka Mwamba wa Kaskazini anaamini walichelewa tu kufika hapo walipofika, lakini pia akawashukuru wale wote waliofanikisha wao kufika pale walipofika.
Ameeleza pia sababu zilizomfanya achelewe kufika hapo na kudai kuwa kutokuwepo umoja kati ya wasanii wa Tanzania kuzisukuma kazi zao ni moja ya kikwazo, na kuutolea mfano umoja uliopo kati ya wasanii wa Nigeria ambao umewawezesha kuiteka Afrika na kuvuka mipaka.
“Sipendi sana kulaumu watu, lakini…unajua wenzetu Nigeria wanatupiga bao kwa sababu wenyewe nchi nzima wanafanya kazi kama timu moja.” Joh Makini ameieleza tovuti ya Times Fm.
Rapper huyo ameeleza pia kuhusu jinsi walivyojipanga kuendelea kumaintain level waliyofikia na mpango wa video ya wimbo wa Gere.
“Sisi Weusi ni watu ambao tunavunja rekodi zetu, ni lazima uweze kuvunja rekodi zako mwenyewe ili uweze kuendelea mbele. Kwa hiyo kazi yeyote nyingine itakayokuja baada ya Gere itavunja rekodi ya Gere. Unajua Nje ya Box imetimiza kile ambacho tuliiagiza kufanya. Kwa hiyo hatuwezi kubaki kwenye Nje ya Box siku zote.
“Nyuma ya Nje ya Box kuna Bei ya Mkaa Video inakuja, kuna Nikumbatie..zote tunaamini zitakuwa na impact tofauti na kazi zilizopita nyuma.” Amefunguka Joh.
Joh na Nikki wa Pili walieleza jinsi ambavyo waliweza kufanikisha kuifikisha Nje ya Box Channel O hadi kupata air time.
“Tulipewa tu connection…kuna mdada alitusaidia tukatafuta connection ya kule akatuma na jamaa wakatutumia form yao tukajibu.” Nikki wa Pili ameeleza.
“Tukatuma kwa email kwa wahusika wanaofanya kazi Channel O, wakaipokea wakaiangalia wakajibu Email kwamba hii kazi tumeipokea na tumeikubali itachezwa hapa Channel O. kwa hiyo I’ts possible, yaani inawezekana kabisa. Cha msingi inatakiwa ianze pale ambapo unafanya video yako mwenyewe kwa sababu wenzetu kule duniani hawashangai tena quality katika hiyo level, kwa sababu quality kila mtu anayo. Lakini ndani ya quality umeweka creativity gani ili mtu aweze kupenda kuitazama kazi “Tulipewa tu connection…kuna mdada alitusaidia tukatafuta connection ya kule akatuma na jamaa wakatutumia form yao tukajibu.” Nikki wa Pili ameeleza.
MKURUGENZI WA BOMBA FM RADIO ZANZIBAR AMEAMUA KUTANUA WIGO WA MZIKI WA ZANZIBAR.SOMA HII

Guru Ramadhani. Mkurugenzi Bomba fm Zanzibar.
Mkurugenzi
mtendaji wa Radio bora hapa zanzibar
Bomba fm Radio GURU RAMADHAN aliwaambia wafanya kazi wake katika kikao
kilichofanyika mapema mwezi huu wa pili.Pamoja na Agenda nyingine ambazo nyeti
zilizojadiliwa pia mkuregenzi huyo alidhamiria kuibua na kuendeleza vipaji vya wanamuziki wa
Zanzibar ambao kwa namna moja ama nyengine vipaji hivyo vinaonekana kupotea
bure .Mkurugenza aliwataka waendesha vipindi vya burudani kulipatia mkazo hilo
na kulitekeleza kwa umakini mkubwa.
Pia
mkurugenzi amefanya mabadiliko ya vipindi kadhaa pamoja maboresho yake,
sikiliza BOMBA FM RADIO zanzibar ili
ujue kilichobadilika mwaka 2014.
Maoni ya
Watangazaji/Angalizo kwa wanamziki wa Zanzibar.
Uptowntz
ilikutana na mtangazaji wa Breakfast Bomba MB The Swaga/Mb Doctor yeye alikua
na haya ya kusema.

MB DOCTOR & PASHA.
MB. Doctor.
Wanamuziki wa Zanzibar wanatakiwa kuboresha nidham zao ili kufikia mafanikio,
pia aliwataka kuacha dharau kwa maana hakuna career ambayo inaweza kusonga
mbele bila nidham ndani yake. Pia aliwataka wasanii kufanya kazi zenye ubora na
kiwango cha juu ili kua na ushindani zaid katika soko la mziki Tanzania.
JABIR.Super
Jay International.Host wa show za kiburu FRIDAY & SAT,DAY NIGHT GROOVE.Alitirirka
ifuatavyo.

JABIR SUPER JAY
Mafanikio
hayapatikani mara moja kama baadhi ya wasanii wanavyodhani hapa Zanzibar.
Inatakiwa kila msanii anaejijua kua anakipaji ambacho kinahitaji kuendelezwa
kama Radio hii ilivyodhamiria kufanya hvyo bac kuchukua jitihada binafsi
kulinda na kutunza kipaji chake ili kupata mafanikio siku za usoni. Super Jay
pia alisisitiza Nidham kwa wasanii. Pamoja na hayo yote alisema kuhusu fursa
hii ambayo wasanii wa Zanzibar wanatakiwa kuitumia bila kuipoteza kwani huu ni
moyo wa uzalendo ambao umeoneshwa na mkurugenzi wa Bomba fm Zanzibar.
Pia
muandishi wa Blog hii alikutana na msanii wa mziki wa kizazi kipya toka maeneo
ya fuoni Dogo fani alipoomuuliza kuhusiana nidham mbovu za wasanii yeye pamoja
na wenzake dogo fani ilikiri kua kweli kuna baadhi ya wasanii wanadharau na
akasema kua wasipobadilika na kujitunza watashindwa kuzitumia fursa kama hizi
ambazo zinatolewa na Bomba fm. Ameenda mbali zaidi na kumpongeza mkurugenzi wa
Bomba fm katika jitihada zake za kuboresha mziki huu.
KAZI KWENU
WASANII KUFANYA KAZI NZURI NA BORA ILI FURSA HII ISIPOTEE BURE.